Subscribe
WANAFUNZI 15 ARDHI TABORA MBARONI KUMNG'OA MENO MLINZI - Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha leo March 07,2026 amethibitisha kukamatwa kwa wanafunzi wa 15 wa Chuo cha Ardhi,tawi la Tabora kwa tuhuma za kumpiga mlinzi wa chuo hicho na kumng’oa meno manne.
Rc Chacha amesema wanachuo hao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kufuatia tukio hilo, huku wengine wawili kati yao wamekutwa na silaha aina ya kisu katika eneo la bweni lao, jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu za chuo.
Aidha ameongeza kuwa jina la mlinzi aliyejeruhiwa limehifadhiwa kwa sasa wakati uchunguzi ukiendelea ambapo ameuagiza uongozi wa chuo hicho kuwasimamisha masomo wanachuo hao pamoja na kuhakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufunguliwa mashitaka.
Hata hivyo Rc Chacha amewataka wanafunzi wengine wa vyuo kuepuka kuiga vitendo vya uhalifu na badala yake kujikita katika masomo yao yaliyowapeleka chuoni hapo.
Comments (0)
Sign in to comment